Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Abdullah Jabri, Katibu Mkuu wa Harakati ya Umma nchini Lebanon, katika mkutano wa fikra na kisiasa ulioandaliwa na Jumuiya ya Vituo vya Utamaduni vya Imam Khomeini (ra) mjini Beirut wakati wa siku za mazishi ya Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei, alisisitiza kwamba; uaminifu kwa mashahidi unadhihirika kwa kushikamana na njia ya jihadi na muqawama, kuimarisha umoja wa Umma wa Kiislamu na kuendelea na juhudi za kuikomboa ardhi na kulinda heshima.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, Sayyid Mohammad Reza Mortazavi, pamoja na kundi la maulamaa, viongozi wa kisiasa, wanazuoni wa masuala ya utamaduni na wanajamii. Hafla hiyo ilifanyika katika Majma' al-Mujtaba (as) iliyoko eneo la Safir, katika vitongoji vya kusini mwa Beirut.
Sheikh Jabri alisema kuwa; mazishi hayo makubwa yaliyounda mandhari ya kipekee yalionesha kwa uwazi kina cha upendo na uaminifu kwa Shahidi huyo, na yakadhihirisha nafasi yake kubwa ndani ya nyoyo za watu huru na mataifa yaliyokuwa yakimwona kuwa alama ya ustahimilivu na kujitolea kwa masuala ya Umma.
Aliongeza kuwa; mahudhurio hayo makubwa ya wananchi katika mazishi hayo ilikuwa ni ujumbe unaosisitiza kwamba viongozi wakubwa huendelea kuishi ndani ya dhamira na nyoyo za mataifa kutokana na kujitolea kwao na misimamo yao.
Sheikh Jabri pia alibainisha kuwa; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeendelea kuwa nguzo kuu ya kuunga mkono kadhia ya Palestina, na imeendelea kuwa msaidizi wa Lebanon katika kukabiliana na uvamizi na mashambulizi ya maadui.
Maoni yako